Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yalaani shambulio dhidi ya msafara wa mazishi Yemen

Ofisi ya haki za binadamu yalaani shambulio dhidi ya msafara wa mazishi Yemen

Ofisi ya haki za binadamu imelaani vikali shambulio la makombora dhidi ya msafara wa mazishi na kuuwa watu 21 na kujeruhi wengine 30 wakiwemo watoto. Shambulio hilo lilifanyika Desemba 27 kwenye jimbo la Al-Dhalai .

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha kuanzishwa kwa kamati ya Rais ya uchunguzi hapo Desemba 28 mwaka 2013 na kutoa wito kwa uongozi waYemenkuhakikisha kwamba uchunguzi huo unakuwa wa haraka, wa kina, unaofuata haki na matokeo yake kuwekwa hadharani.

Pia ofisi hiyo imeitaka serikali ya Syria kuhakikisha wahusika wa shambulio hilo wanajibishwa kwa mujibu wa sheria.