Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yatafuta dola bilioni moja kwa ajili ya watoto wa Syria:UNHCR/UNICEF

Mashirika ya UM yatafuta dola bilioni moja kwa ajili ya watoto wa Syria:UNHCR/UNICEF

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamezindua kampeni ya kuchangisha dola bilioni moja ili kutoa msaada na kuwalinda zaidi ya watoto wa Syriamilioni nne waliotawanywa na machafuko ndani ya nchi au wanaoishi katika mataifa jirani kamawakimbizi. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  yamesema mustakhbali wa watoto wa Syria unatoweka na bila kuchukuliwa hatua kubwa na za haraka za kimataifa  kusaidia basi watoto wengi watakabiliwa na maisha ya adha, yasiyo na matumaini na mustakhbali duni.

Mashirika hayo yamesema watoto ndio wamekuwa wahanga wakubwa kuliko mtu yeyote katika vita vita vyaSyria, wakishuhudia familia zao na jamaa zao wakiuawa, wakikabiliwa na mifumo mibaya zaidi ya unyonyaji ikiwemo ajira kwa watoto, kuingizwa vitani na makundi yenye silaha, ndoa za mapema na ukatili wa kijinsia.

Fedha zitakazochangishwa na kampeni hiyo iitwayo “Hakuna kizazi kitakachopotea”zitaingizwa katika mipango ya kutoa elimu, kuwalinda na unyonyaji, ukatili na ghasia, huduma za kisaikolojia, msaada na kuwapa fursa ya kuchangamana katika jamii na utulivu. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MELISA FLEMING

 “ Sehemu ya tatizo ni nchi kuzidiwa , kwa mfano Lebanon mfumo wa shule umefurika, hakuna nafasi za kutosha na tayari wanasoma kwa awamu mbili, hivyo kuna kazi kubwa ya kuendeleza mfumo huo na kujenga miundombinu ya elimu hususani nchini Lebanon, lakini pia Jordan na bila shaka ndani ya Syria ambako inakadiriwa kuwa nusu ya watoto wa shule hawahudhurii tena masomo na idadi kubwa ya shule zimeharibiwa. Hivyo ni mradi mkubwa unaohitaji ufadhili.

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa zaidi ya watoto waSyriamilioni moja wanaishi kama wakimbizi katika nchi jirani huku wengine milioni 3 ni wakimbizi wa ndani nchiniSyria.