Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atuma mialiko kwa washiriki kwenye kongamano kuhusu Syria

Ban atuma mialiko kwa washiriki kwenye kongamano kuhusu Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametuma nyaraka za mialiko kwa WaSyria na washiriki wa kimataifa kwenye kongamano kuhusu Syria, ambalo linatarajiwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi kuanzia Januari 22, 2014.

Orodha ya washiriki kwenye kongamanohiloiliamuliwa mnamo tarehe 20 Disemba kwenye mkutano ulohusisha Marekani, Urusi na Umoja wa Mataifa.

Kongamano hilo limetokana na juhudi muhimu zilizotangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, mnamo Mei 7, mwaka 2013 mjini Moscow. Kongamano hilo linalenga kuwaleta wawakilishi wa kuaminika wa serikali na makundi ya upinzani kwenye meza ya mawasiliano, ili kuumaliza mgogoro uliopo Syria na kuanza kipindi cha mpito wa kisiasa utakaozingatia utekelezaji kikamilifu kwa makubaliano yaGenevaya tarehe 30 Juni mwaka 2012.

Bwana Ban analiona kongamanohilokama fursa ya kipekee ya kumaliza ghasia na kuhakikisha kuwa amani inarejeshwa, huku makubaliano ya Geneva yakitekelezwa kwa njia inayoridhisha matakwa ya raia wote wa Syria.