Usawa wa kijinsia wamulikwa nchini Tanzania

3 Januari 2014

Mwaka 2000 wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha malengo ya maendeleo ya Milenia, malengo yako manane na lengo namba Tatu ndiyo mada kuu ya Makala yetu wiki hii.Lengo hilo ni kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake. Masuala yanayomulikwa hapa ni kuondoa tofauti ya uandikishaji watoto wa kike na kiume mashuleni, uwiano wa ajira nje ya sekta ya kilimo na tatu ni ushiriki wa wanawake kwenye maamuzi ikiwemo kuingia katika mabunge na kushika nafasi za kisiasa. Miongoni mwa nchi zilizoridhia malengo hayo ni Tanzania. Basi hii leo katika Makala ya wiki, Tamimu Adam wa Radio WAshirika Jogoo FM kutoka Ruvuma Tanzania anamulika utekelezaji wa suala hilo ikiwa zimesalia chini ya siku 1000 kufikia ukomo wa malengo hayo.

(PKG YA TAMIMU)