Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa vitatu vya surua vyabainika CAR na kampeni ya chanjo yaanza:WHO

Visa vitatu vya surua vyabainika CAR na kampeni ya chanjo yaanza:WHO

Shirika la afya dunini WHO limesema visa vitatu vya surua vimebainika katika makambi mawili ya wakimbizi wa ndani karibu na uwanja wa ndege wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Kufuatia hali hisho WHO, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF na shirika la madaktari wasio na mipaka MSF wameanza Ijumaa ya leo kampeni ya chanjo nchini humo. Kituo cha wakimbizi wa ndani cha Don Bosco mjini Damala pia kumeaarifiwa visa vitano. Maeneo 13 yameandaliwa kwenye uwanja wa ndege nchini humo maalumu kwa ajili ya kuendesha chanjo hiyo. 
Kwa mujibu wa mashirika hayo matatu kampeni ya chanjo itatumu kwa siku 3 hadi 5. Wadau wengine wa mashirika hayo wamejitolea pia kusaidia kampeni ya njacho ili kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa.