Hali bado ni tete CAR: UNHCR

3 Januari 2014

Hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati bado ni tete, huku kutokuwepo na usalama kunasababisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu kuwa vigimu zaidi limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.  Taarifa kamili na Flora Nducha.

 (TAARIFA YA Flora Nducha)

Kwa mujibu wa shirika hilo idadi ya wakimbizi wa ndani inaongezeka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na saSA IMEPITA 935,000. Limeongeza kuwa mashambulizi ya kulenga dhidi ya raia , uporaji na kuwepo kwa silaha miongoni mwa maeneo ya wakimbizi wa ndani limedhoofisha kabisa uwezo wa mashirika ya misaada ya kibinadamu kuwafikia maelfu ya watu wanaohitaji msaada. Babar Baloch  ni msemaji wa UNHCR

 (SAUTI YA Babar Baloch)

 “Mashambulizi yanayolenga raia, uporaji na uwepo wa vikundi vilivyojihami kwa silaha katika baadhi ya maeneo vimekwamisha kwa kiasi kikbwa mashirika a misaada kufikia raia wanaotaka misaada. Wafanyakazi wetu wameripoti kuwa wananchi wamesaka hifadhi maporini kwa hofu ya mapigano mapya. Kuzorota kwa usalama, pamoja na umbali mrefu kwenda kambi za wakimbizi wa ndani nje ya mji mkuu Bangui na barabara mbovu vinazidi kukwamisha juhudi za UNHCR kufikia watu waliokimbia mapigano.”