Katibu Mkuu alaani shambulio la Beirut, Lebanon

2 Januari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani vikali shambulio la leo kwenye kitongoji cha Haret Hreik, kusini mwa mji mkuu wa Lebanon,Beirut. Bwana Ban amekaririwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa akieleza kuwa mlipuko huo wa  bomu kwenye gari uliosababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi umetokea siku chache baada ya shambulio lingine la aina hiyo wiki moja iliyopita.

Amesema matukio hayo yanadhihirisha mazingira yanayotia shaka juu ya utulivu nchiniLebanon. Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande zote kujizuia na wananchi wawe kitu kimoja kuunga mkono taasisi za serikali hususan jeshi na vikosi vya usalama wakati huu vinapojitahidi kukabiliana na ugaidi.

Bwana Ban ametuma rambirami kwa wafiwa na serikali yaLebanonhuku akitaka ahueni ya haraka majeruhi. Halikdhalika amezungumzia umuhimu wa wahusika wa matukio hayo kufikishwa mbele ya sheria mapema iwezekanavyo.