Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vitokanavyo na ugaidi vyaongezeka Iraq, UM waonya

Vifo vitokanavyo na ugaidi vyaongezeka Iraq, UM waonya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMA, umetoa takwimu zinazoonyesha kuongezeka kwa mauaji yatokanayo na ugaidi kwa mwaka 2013 ambapo kwa mwezi December pekee watu 759 waliuwawa huku 1345 wakijeruhiwa.

Katika orodha hiyo ya vifo UNAMA inasema  raia ni 661 wakiwemo polisi jamii 175 huku pia katika idadi ya wale waliojeruhiwa raia ni 1201 na polisi jamii wakiwa 258. Takiwmu hizo pia zinaonyesha kuwa wanausalama  98 kutoka vikosi vya jeshi waliuwawa na 144 kujeruhiwa. Mwezi May umeripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo kwa mwaka huu pekee raia 3154 waliuwawua katika ghasia za kigaidi na wengine 2191 kujeruhiwa.

Hii inamaamisha mwaka 2013 umeshuhudia idadi kubwa ya vifo na majeruhi watokanao na matukio ya ugaidi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kufuatia hilo msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov amesema hizo ni habari mbaya zinazoonyesha umuhimu kwa serikali ya Iraq kushughulikia kwa haraka chanzo cha ghasia nchini humo ili kukabiliana na mauaji hayo.