Hali ya mtoto wa kwanza kuzaliwa mwaka mpya huko Tacloban si nzuri

2 Januari 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu, UNFPA limesema hali ya kiafya ya mtoto wa kwanza kuzaliwa mwaka mpya 2014 huko Tacloban, nchini Ufilipino si nzuri pamoja na mama yake.

Shirika hilo linasema mama huyo Vivian Aplaca alijifungua salama kwa upasuaji kwenye kituo cha Visayas ambacho kilipatiwa vifaa vya kisasa na UNFPA baada ya kimbunga Haiyan kupiga na kusambaratisha miundombinu ya afya.

Hata hivyo saa chache hali ya mtoto ilibadilika na hadi sasa yuko kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na mama yake anakabiliwa na shinikizo la damu. Hivi sasa madaktari kwenye kituo hicho wanafanya kila jitihada kuokoa maisha ya mama na mtoto.

UNFPA inakadiria kuwa mwaka huu pekee eneo lililokumbwa na kimbunga huko Tacloban, litakuwa na vizazi Laki Tatu na Elfu Sabini na Tano.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter