Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini iko njiapanda, hatma yake iko mikononi mwa wanasiasa: UNMISS

Sudan Kusini iko njiapanda, hatma yake iko mikononi mwa wanasiasa: UNMISS

Sudan Kusini iko njiapanda lakini bado kuna fursa ya kuepusha mwendelezo wa ghasia na mapigano, amesema Hilde Johnson mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo na pia mkuu wa ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani  UNMISS. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Katika salamu zake za mwaka mpya kutokaJuba, Bi. Johnson amesema matarajio yote ya kuendeleza nchi hiyo kiuchumi yaliyofikiwa takribani mwezi mmoja uliopita katika kongamano la uwekezaji sasa yametumbukia. Amesema ni matumaini yake kuwa mwaka huu utarejesha matumaini ambayo yalianza kuonekana ndani ya taifahilochanga. Hata hivyo amesema mustakhbali waSudanKusini uko mikononi mwa viongozi wa kisiasa, Rais Salva Kiir, makamu wake wa zamani, Riek Machar na wananchi kwa ujumla.

(Sauti  ya Hilde)

 

“Ninatoa wito kwa wananchi wote wa Sudan kusini wasaidie kuleta utulivu. Wajizuie kutumia lugha ya uchochezi au chuki. Natoa wito kwa viongozi wa nchi hii changa na vyama vyote vya kisiasa, vikundi  pamoja na viongozi wa kijamii  kujizuia na vitendo ambavyo vinaweza kuchochea vita vya kikabila na kuchochea ghasia. Nawasihi raia wote, ninyi viongozi wa nchi hii  kuzuia vitendo vyovyote vya ghasia dhidi ya  jamii yoyote bila kujali ni nani na wanakotoka."

Tayari pande mbili hizo zinazokinzana zimetuma wajumbe wao hukoAddis AbabaEthiopiakwa ajili ya mazungumzo yanayoratibiwa na nchi za IGAD. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu usaidizi wa kibinadamu, OCHA linasema hadi sasa zaidi ya watu 190,000 wamepoteza makaziyaonchini humo. Hata hivyo waliofikiwa na misaada ni Laki Moja na ElfuSaba.