Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasudan Kusini 7600 waingia Uganda kufuatia mapigano nchini mwao

Wasudan Kusini 7600 waingia Uganda kufuatia mapigano nchini mwao

Mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini yamesababisha raia kuendelea kukimbia nchi hiyo na ripoti za hivi karibuni zinakariri kuwa zaidi ya raia 7600 wamekimbilia nchiniUgandawakati huu ambapo Umoja wa Mataifa na nchi za Afrika zinaendelea na jitihada za kupata suluhu la kisiasa kwenye mzozo huo. Kwa tarifa kamili, tungane na John Kibego wa redio washirika ya Spice FM,Uganda.

(Tarifa ya John Kibego)

Wakimbizi hao kutoka majimbo tofauti ya Sudan Kusini wamekuwa wakiija kwanzia tarehe kumi na sita mwezi Disemba, siku moja baada ya makabiliano kati wa wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa makamu rais Riek Machar, na wale wa raisi Salva Kiir katika mji mkuu wa nchi hiyo,Juba.

Douglas Asiimwe, afisa mwandamizi wa kutetea wakimbizi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu amesema, wakimbizi hao wamahifadhiwa kwenye kambi tatu za wakimbi.

Amesema wakimbizi 3553 wao wamesajiliwa katika kambi ya Agago wilayani ya mpakani ya Adjumani. Wengine 3520 wamesajiliwa katika kambi ya Rhino wilayani Arua.

Nayo kambi ya Kiryandongo wilayani Kiryandongo imepokea wakimbizi 532.

Bwana Asiimwe amesema, wanatarajia kupokea wakimbizi zaidi kwa sababu hali bado ni tete Sudan Kusini hususani katika majimbo yenye mafuta.