Hali si shwari katika taifa changa zaidi duniani:Sudan Kusini

31 Disemba 2013

Ni wimbo wa taifa wa Sudan Kusini, ulipoimbwa kwa mara ya kwanza, kukaribisha kuzaliwa kwa taifa jipya kabisa duniani. Julai 9, mwaka 2011,ilikuwa ni siku ya sherehe na matarajio makubwa, kama alivyoeleza Katibu Mkuu Ban Ki-Moon wakati huo katika hotuba yake

(Sauti ya Ban)

Ban pia aliwakumbusha watu wa Sudan Kusini kuhusu wajibu wao

(Sauti ya Ban)

Mwaka huu, Sudan Kusini imesherehekea mwaka wa pili wa uhuru wake tangu tarehe hiyo, mnamo Julai 9. Lakini siku chache baadaye mwezi huo wa Julai, Rais Salvar Kiir alivunja baraza lake la mawaziri na kumwachisha kazi makamu wake, Riek Machar.

Miezi minne baadaye, ndoto za taifahilojipya zimetumbukia mashakani. Mnamo Disemba 15, ripoti za jaribio la kuipindua serikali ya Rais Kiir zilipokelewa kwa masikitiko makubwa, na haraka, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likafanya kikao cha dharura. Gerard Araud amekuwa rais wa Barazahilomwezi huu wa Disemba

 (Sauti ya Araud)

Kufikia sasa, Ofisi ya Kuartibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, imesema takriban watu 180,000 wamelazimika kuhama makwao,  zaidi ya wakiwa wanapewa hifadhi na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS.

Mnamo wiki ilopita, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNMISS, Hilde Johnson, alipaaza sauti ya kusikitikia hali ya Sudan Kusini

(Sauti ya Hilde)

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 1,000 huenda wameuawa katika mapigano hayo ya kisiasa ambayo baadaye yalichukua mkondo  wa mapigano ya kikabila.

Akizungumza kuhusu mzozo huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Muunganowa Nchi za Afrika, Dkt Salim Ahmed Salim alikuwa na mtazamo huu

 (Sauti ya DKT SALIM)

Mwaka wa 2013 umekuwa ni mwaka wa kukaribisha tena taabu ambazo watu wa Sudan Kusini walidhani zilimalizika pale walipopata uhuru, na kuuimba wimbo huu kwa matumaini makubwa

 (Wimbo)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter