Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya viongozi wa Kenya itasalia ICC, Afrika haijakata tamaa

Kesi ya viongozi wa Kenya itasalia ICC, Afrika haijakata tamaa

Kesi inayowakabili  viongozi wa Kenya, Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto mahakama ya kimataifa ya uhalifu , ICC ilitikisa mwaka 2013 ambapo Umoja wa  Afrika (AU) uliwasilisha rasmi ombi kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi yao. Ombihilohata hivyo lilitupiliwa mbali baada kukosa kura zinazotakiwa na hivyo kuashiria kuwa kesi itaendeleakamailivyopangwa. Balozi  Macharia Kamau Mwakilishi wa kudumu waKenyakwenye Umoja wa Mataifa alizungumzia suala hilo.

(Sauti Kamau)