Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

2013 ulileta matumaini kwa wakazi wa mashariki mwa DR Congo

2013 ulileta matumaini kwa wakazi wa mashariki mwa DR Congo

Machi 28 2013, itaingia katika vitabu vya historia siyo tu kwa DR Congo bali pia kwa ulimwengu mzima kwani Baraza la Usalama lilipitisha azimio namba 2098 lililoridhia kuundwa kwa brigedi maalum ya MONUSCO ya kuingilia kati mashambulizi au kushirikiana na serikali ya DRC kupunguza uwezo wa waasi na vitisho kwa usalama wa raia na hatua hiyo ilitokana na kurejea kwa mapigano kulikosababisha kupitishwa kwa mpango wa amani uliotiwa saini huko Addis Ababa mwezi Februari. Azimio limezaa matunda na waasi wa M23 wamefurushwa kutoka Mashariki mwa nchi hiyo, amani imerejea na miradi ya miundombinu ya kijamii imeanza kutekelezwa na nguvu imeelekezwa kufurusha waasi wa FDLR. Martin Kobler Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu huko DR Congo na Mkuu wa MONUSCO.

 (Sauti ya Kobler)