Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama CAR yaendelea kuwa tete, maelfu waendelea kukosa makazi

Hali ya usalama CAR yaendelea kuwa tete, maelfu waendelea kukosa makazi

Hali ya usalama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kuwa tete hali ambayo imesababisha kuzuka kwa wimbi kubwa la raia wanaopoteza makazi  katika mji mkuuBangui. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika ka Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA. George Njogopa na taarifa zaidi.

Idadi ya watu waliokosa makazi katika mji waBanguiimeendelea kuongezeka na sasa taarifa zinasema kuwa idadiyaoinakadiriwa kuzidi watu 370,000 ikiwa ni ongezeko la mara kadhaa ikilinganishwa na ile iliyorekodiwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambayo ilikuwa ni 214,000.

Wakati hali ikiwa hivyo, Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutolewa kiasi cha dola za Marekani milioni 152 ili kuyakwamua maisha ya waathirika hao katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo kuanzia mwaka 2014.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kibinadamu OCHA linasema kuwa kiasi cha watu 800,000 nchini kote wamekosa makazi na kiasi cha watu milioni 2.2 wanahitaji misaada ya haraka.

Duru zaidi za habari zinaeleza kwamba katika uwanja wa ndege waBanguikuna idadi ya watu wanaokadiria kufikia 70,000- 100,000 ambao wameomba hifadhi kwenye eneohilohuku mashirika ya misaada ikiwemo lile la mpango wa chakula WFP yakijikwamua kwa hali namaliili kuwafikishia misaada. Elizebeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(Sauti ya Byrs)