Watoto wanauawa kikatili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati:UNICEF

31 Disemba 2013

Takriban watoto wawili wanaripotiwa kuuawa kwa kukatwa vichwa tangu kuanza kwa ghasia kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  mapema mwezi huu.

Mjumbe wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Jamahuri ya Afrika ya kati Souleymane Diabate anasema kuwa dhuluma zinazoendehswa dhidi ya watoto ni za kutisha ikiwemo kuingizwa jeshini na pia wakiwa wanalengwa wakati wa  wa kulipiza kisasi.

UNICEF na washirika wake wamethibitisha kuuawa kwa karibu watoto 16 na kujeruhiwa kwa karibu ya  wengine 60 tangu ghasia zianze kushuhudiwa mjiniBanguitarehe tano mwezi huu.

Karibu watu 370,000 ikiwa ni nusu ya watu wote kwenye mji mkuu Bangui wamekimbia makwao majuma kadha yaliyopita huku watu wengine 785,000  wakihama makwao sehemu tofauti za nchi tangu kuanza kwa mapigano karibu mwaka mmoja uliopita.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter