Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kumaliza mzozo Sudan Kusini zahamia Ethiopia

Harakati za kumaliza mzozo Sudan Kusini zahamia Ethiopia

Nchini Sudan Kusini  yaripotiwa mapigano makali yanaendelea kwenye mji wa Bor katika jimbo la Jonglei ambako hivi karibuni kuliripotiwa kuwa majeshi ya serikali yamejizatiti kuutwaa mji huo kutoka kwa waasi. Waasi hao yasadikiwa ni wafuasi wa Makamu wa Rais wa zamani Riek Machar. Wakati hayo yakiendelea hukoAddis AbabaEthiopiakunafanyika mkutano kati ya ujumbe wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Riek Machar, mazungumzo yaliyoratibiwa na mamlaka ya IGAD. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS unasema hali ya kibinadamu inatia shaka.