Skip to main content

Katibu mkuu azungumza na Rais Putin kuhusu mashambulio huko Volgograd

Katibu mkuu azungumza na Rais Putin kuhusu mashambulio huko Volgograd

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu an Rais Vladmir Putin wa Urusi kuhusu mashambulio mawili kwenye mji wa Volgograd jana na leo ambapo ametuma salamu za rambirambi kwa familia na kwa serikali ya nchi hiyo. Bwana Ban amesisitiza umuhimu kwa ushirikiano thabiti wa kimataifa wa kukabiliana na ugaidi huku akitaka wahusika wafikishwe mbele ya sheria. Kwa upande wake Rais Putin ameshukuru kwa risala za rambirambi kutoka kwa Bwana Ban akisema zimepokelewa kwa moyo mkunjufu na wananchi wa Urusi. Halikadhalika amepongeza hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu jitihada za kutokomeza uhalifu wa kupangwa na ugaidi akimhakikishia Bwana Ban kuwa Urusi itazingatia sheria za kimataifa kuwafikisha watuhumiwe mbele ya vyombo vya haki.

Ban na Putin kando mwa mashambulio ya Volgograd wamejadili pia masuala ya Syria ikiwemo mkutano wa pili wa amani huko Uswisi tarehe 22 mwezi ujao na ule wa usaidizi wa kibanadamu kuhusu Syria tarehe 15 mwezi huo huko Kuwait.