Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yachukua hatua kufuatia mapigano huko DRC

MONUSCO yachukua hatua kufuatia mapigano huko DRC

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo kumeripotiwa mapigano kwenye mji mkuu Kinshasa, Lubumbashina Kindu kati ya jeshi la serikali na watu wasiofahamika waliokuwa wamejihami ambapo ujumbe wa umoja wa mataifa nchini humo, MONUSCO umechukua hatua kuhakikisha usalama kwa watendaji na vikosi vyake kwenye maeneo hayo.

Msemaji waUmoja wa Mataifa Martin Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, kuwa wakati wa mapigano hayo kwenye uwanja wa ndege mjini Kinshasa, mfanyakazi mmoja wa Umoja huo ambaye ni raia wa DRC alijeruhiwa. Hata hivyo hali ya utulivu imerejea.

(Sauti ya Martin)

Ujumbe huo umeripoti kuwa utulivu umerejea Lubumbashi na Kindu ambapo vikosi vya MONUSCO vilivyopiga kambi kwenye uwanja wa ndege vilikabiliana na washambuliaji waliokuwa na silaha. Mpaka sasa utambulisho na lengo la washambuliaji hao haijafahamika.”