Kikao cha 56 cha Mkataba kuhusu Haki za Watoto kufanyika Geneva Januari 13-31, 2014

Kikao cha 56 cha Mkataba kuhusu Haki za Watoto kufanyika Geneva Januari 13-31, 2014

Kikao cha sitini na tano cha Kamati ya Mkataba kuhusu Haki za Watoto kitafanyika kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuanzia tarehe 13 hadi tarehe 31 Januari hapo mwakani. Katika kikao hicho, ripoti za hali ya haki za watoto katika nchi mbali mbali wanachama zitatolewa.

Miongoni mwa ripoti zitakazotolewa ni ile inayohusu hali ya haki za watoto nchini Kongo Brazzaville, ambayo bado imeghubikwa na umaskini, na hivyo kupunguza uwezo wa kuwafikishia huduma kama vile za afya, elimu, maji safi na lishe.

Hata hivyo, ripoti hiyo inasema kuwa hatua zimepigwa katika kutekeleza mkataba kuhusu haki za watoto kwa ujumla nchini humo, hususan katika kuzingatia vipengee vyake, kutunga sera na kuendeleza mfumo wa haki. Kumekuwa na mikakati pia ya kuwalinda watoto walio hatarini, kama vile wenye ulemavu, kuzuia ukatili, utelekezaji, usafirishaji haramu na unyanyasaji wa watoto.