Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Cambodia yajindaa kutoa hukumu nyinginie mwakani

Mahakama ya Cambodia yajindaa kutoa hukumu nyinginie mwakani

Mahakama ya kimataifa iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza uhalifu wa kibinadamu uliofanyika Cambodia katika kipindi cha mwaka 1975 hadi 1979 inajiandaa kutoa hukumu yake hapo mwakani ikiwa imepita miaka sita tangu kuasisiwa wake.

Hadi sasa mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imemhukumu mtu mmoja kwenda jela kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia.

Kaing Guek awali alihukumiwa miaka 35 lakini baadaye hukumu hiyo ilibadilishwa na kuwa kifungu cha maisha. Watu zaidi ya milioni 1.7 wanasadikika walipoteza maisha wakati wa utawala wa kidhalimu wa wakati huo wa Khmer Rouge ulipotenda vitendo vya kinyama.

Hapo mwakani mahakama hiyo inakusudia kutoa hukumu kwa viongozi wengine watatu ambao wanadaiwa kushiriki wal kwenye vitendo vya kinyama.