Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la kigaidi Beirut, Baraza la Usalama laani vikali

Shambulio la kigaidi Beirut, Baraza la Usalama laani vikali

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la kigaidi lililofanywa Ijumaa huko mjini Beirut, Lebanon lililosababisha vifo vya watano akiwemo Waziri wa zamani nchini humo Mohammed Chatah na majeruhi kadhaa.

Wajumbe pamoja na kulaani wametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na serikali yaLebanonhuku wakisisitiza msimamo wao wa kushutumu jaribio lolote lile la kutibua utulivu nchini humo kwa njia ya vitisho vya kisiasa. Katika taarifayaoiliyotolewa leo, wametaka tabia hiyo kukoma mara moja na kusema kuwa vitendo vya kigaidi ni moja ya tishio kubwa la amani na utulivu duniani na kwamba vitendo hivyo haviwezi kuhalalishwa kwa misingi yoyote ile bila kujali nani anatekeleza na anapotekelezea.

Wametaka wahusika wafikishwe mbele ya sheria huku wakirejelea taarifa ya Rais wa barazahiloya tarehe 10 Julai mwaka huu inayosihi wananchi waLebanonkulinda umoja wao pindi kunapoibuka mbinu yoyote ya kutibua utulivu nchini humo. Wajumbe wa baraza la usalama wametaka pande zote ikiwemo wanasiasa kuepuka kujihusisha na mzozo waSyriakwa mujibu wa azimio la Baabda.