Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yashangazwa na mashambulizi yanayolenga kambi ya Hurriya mjini Baghdad

UNHCR yashangazwa na mashambulizi yanayolenga kambi ya Hurriya mjini Baghdad

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeshutumu shambulizi lililofanywa eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Baghadad ambapo maroketi kadha yaliyofyatuliwa yalianguka kwenye kambi ya Hurriya ambapo watu watatu waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Awali kambi ya Hurriya ilikuwa imeshambuliwa mara kadha mashambulizi ambayo yemelaaniwa na UNHCR.

UNHCR imeelezea wasi wasi wake kuhusiana na usalama wa wenyeji wa kambi ya Hurriya na inatoa wito kwa serikali ya Iraq kufanya hima na kuhakikisha kuwa usalama umeboreshwa kwenye kambi hiyo ili kuhakikishia usalama wa wakazi wake.