Watu wengine wanne wakumbwa na virusi vya Corona Mashariki ya Kati

27 Disemba 2013

Shirika la afya ulimwenguni WHO limepokea ripoti inayodhibitisha kuwepo kwa watu wengine wanne wenye virusi vyaCoronakatika eneo la Mashariki ya Kati na jitihada zimeanza kuchukuliwa kukabiliana na tatizo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za awali, wanawake wawili ambao ni wafanyakazi wa afya kutoka Riyadhi wamegundulika kuwa wamekubwa na virusi hivyo. Hata hivyo bado hawajaonyesha dalili zozote.

Mtu wa tatu ametajwa kuwa mwanaume wa miaka 53 wa hukoRiyadhambaye anaelezwa kuwa katika hali mbaya.Alilazwa hospitalini tangu Novemba 26 na hadi sasa yupo katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa ziada. Mtu wa nne ni mwaume mwenye umri wa miaka 73 ambaye hata hivyo aliaga dunia Disemba 18 .

Tangu kuanzia Septemba mwaka uliopita,WHO imepokea ripoti zinaonyesha kuwa watu 170 wamekumbwa na virusi hivyo duniani kote ikiwemo vifo 72.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter