Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 31 wazaliwa nchini Sudani Kusini katika kambi ya UNMISS

Watoto 31 wazaliwa nchini Sudani Kusini katika kambi ya UNMISS

Licha ya madhila ya mapigano wanayokumbana nayo raia wa nchi hiyo, wakati wa krismasi watoto 31 walizaliwa katika kliniki inayohudumiwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS mjini Juba . Hatua hiyo iliiibua furaha kwa  wauguzi kama meja Nour Sarin

 (Sauti)

"Ndiyo ninafuraha sana leo. Nimezalisha watoto wa kike watatu katika hospitali ya Cambodia ya daraja la tatu. nina furaha sana. Wamezaliwa leo siku ya krismas, nina furaha saana.

Inatarajiwa kuwa idadi zaidi ya watoto watazaliwa katika kambi hii ya muda ya UNMISS ambapo maelfu ya raia wamejihifadhi.