UNICEF yasaka mabilioni ya dola kuwanusuru watoto Syria

26 Disemba 2013
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF linahitaji dola Milioni 835 kwa mwaka ujao ili kufanikisha mpango wa utoaji misaada ya dharura kwa mamia ya watoto walioathirika na mapigano nchini Syria. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Ripoti ya Assumpta)

Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 77 ikilinganishwa na ombi la mwaka uliopita, lakini ni kikubwa zaidi kuwahi kuombwa na moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa katika historia ya miaka 67 ya kuasisiwa kwa Umoja huo.

Mapigano yanayoendelea sasa nchini Syria yamesababisha mamia ya raia kupoteza makazi huku hali ya uchumi ikiendelea kuanguka.Inakadiriwa kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi hapo mwakani. Nchini Syria kwenyewe  UNICEF inasema kuna watoto zaidi ya milioni 4 wanaohitaji misaada ya haraka na wengine milioni Moja wako nje ya Syria.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kampeni ya kusaka fedha hizo,Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Yoka Brandt alisema watoto wanaendelea kutaabika kutokana na misukosuko inayoendelea duniani na kwamba zaidi ya watoto milioni 14 wamekwama kwenye maeneo mbalimbali wakihitaji usaidizi.

Amesema watoto hao wako Syria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako kuna machafuko yanayoendelea bila kusahau Ufilipino.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter