Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola Milioni 116 zahitajika kunusuru maisha ya wananchi Sudan Kusini

Dola Milioni 116 zahitajika kunusuru maisha ya wananchi Sudan Kusini

Huku mgogoro wa kivita ukiendelea kutokota Sudan Kusin, mashirika ya kutoa misaada ya kiutu yanasema kuwa yanahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 116 katika kipindi cha sasa hadi mwezi Mechi mwakani ili kuwawezesha watu walioathirika na machafuko hayo kurejea kwenye hali zao za kawaida.Mahitaji muhimu yanayohiyajika sasa ni pamoja na kuandaa mpango wa dharura kwa wakimbizi zaidi ya 200,000 kutoka Sudan na wa Sudan Kusini. George Njogopa na ripoti kamili

Mashirika hayo ya misaada ya kiutu yanasema kuwa yanahitaji kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutengeneza mifumo ya maji safi na salama, vituo vya afya, makazi ya muda, na usambazaji wa chakula kwa waathirika wa mapigano.

Pia kunahitajika mpango maalumu kwa ajili ya kuwakirimu na kuwalinda makundi ya watu yanayoshinda kujimudu ikiwemo pia manusura wa machafuko hayo.

Hadi sasa mashirika hayo ya misaada yamejitahidi kuzikabili baadhi ya changamoto zinazojitokeza ikiwemo kuwahudumua zaidi ya wakimbizi 58,000 waliopewa hifadhi kwenye kambi za Umoja wa Mataifa.

Mratibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA, Toby Lanzer ameelezea mazingira magumu wanayokumbana nayo wananchi wa taifa hilo changa na kwamba katika kipindi cha siku chache zilizopita zaidi ya wananchi 90,000 walipoteza makazi.