Ban awatumia ujumbe wananchi wa Sudan Kusini

25 Disemba 2013

Sauti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon katika ujumbe wake kwa njia ya radio na video kwa wananchi wa Sudan Kusini ambao kwa zaidi ya wiki moja sasa wamekumbwa na sintofahamu ya hatma ya Taifa lao changa kufuatia mapigano  yaliyozuka na kusababisha raia Elfu 81 kupoteza makazi yao.Kwanza Ban kwa mara nyingine tena akatoa hakikisho..

“Nataka niwahakikshie kuwa Umoja wa Mataifa uko nanyi wananchi wa Sudan  Kusini wakati huu mgumu. Sudan Kusini iko katika kitisho! Lakini Sudan Kusini haiku peke yake yake.”

Katibu Mkuu akaelekeza ujumbe kwa viongozi nchiniSudanKusini..

“Kwa mara nyingine tena, nawasihi viongozi nchini humo kumaliza tofauti zao kwa amani na kutambua wajibu wao wa kulinda raia. Nimewaonya kuwa wote watawajibika kwa uhalifu ambao watapatikana nao.”

Bwana Ban akaenda mbali zaidi kukumbusha mwezi Julai mwaka 2011 alipoungana na wananchi wa Sudan Kusini mjiniJubakusherehekea siku kuu ya Uhuru na kusema kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa pamoja na nchi hiyo kukabiliana na changamoto za taifa jipya hivyo basi…

“Tunaimarisha uwepo wa Umoja wa Mataifa na tutafanya kwa uwezo wetu wote kusitisha ghasia na kuwasaidia kujenga mustkhbali bora kwa wote.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter