Wataalamu waeleza kutoridhika na mbinu za uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi

24 Disemba 2013

Wataalamu wawili huru wa masuala ya kibidamamu wa Umoja wa Mataifa hii leo wamekaribisha kuchapishwa kwa ripoti ambayo ni uchunguzi  unaohusu mateso na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu uliofanywa na uingereza dhidi ya watu wanaozuiliwa nchi za ng’ambo kwa minajili ya vita dhidi ya ugaidi.

Hata hivyo mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya mateso Juan E. Mendez  na mjumbe anayehusika na masuala ya kulinda haki za binadamu wakati wa kukabiliana na ugaidi Ben Emmerson wameelezea wasi wasi  wao kuwa uchunguzi huo utakabidhiwa kamati zinazohusika na ujasusi pamoja na usalama.

Mendez ameikumbusha serikali ya uingereza kuwa ni wajibu wake chini ya mkataba wa Umoja  wa Mataifa unaopinga mateso kuwa kila serikali ni lazima ichukue hatua ikiwa kuna uwezekano kuwa dhuluma zilindeshwa na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter