Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya raia 81,000 Sudan Kusini wamekosa makazi-OCHA

Zaidi ya raia 81,000 Sudan Kusini wamekosa makazi-OCHA

Idadi ya watu waliopoteza makazi huko Sudani Kusini kutokana na machafuko yanayoendelea inakadiriwa kufikia jumla 81,000, lakini hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa idadi hiyo ikaongezeka.

Wakati hali ya upatikanaji wa misaada ya kiutu kwa raia zaidi ya 45,000 ambao wameomba hifadhi katika kambi ya Umoja wa Mataifa siyo ya kuridhisha kutokana na kukosekana kwa hali ya usalama.George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Kumekuwa na jitihada kubwa za usambazaji wa huduma za kibinadamu kwa waathirika wa machafuko hayo walioomba hifadhi kwenye kambi za Umoja wa Mataifa zilizoko katika maeneo ya Juba.

Lakini hata hivyo pamoja na juhudi hizo za kuwakirimu raia hao wapatao 20,000 walioko kwenye kambi mbili, bado kuna hali ya mkwamo unaojitokeza kutoka na kitisho cha usalama ambacho kimekwaza operesheni za usambazaji wa chakula.

Zaidi ya familia 2,2000 zilizoko huko Juba zilisambaziwa msaada wa chakula hapo Disemba 22  na 23  wakati msaada mwingine wa chakula ilizifikia familia 7,000 ambazo zimepata hifadhi kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Bentiu.

Duru kutoka kwa mashirika ya utoaji misaada zimearifu kuwepo kwa huduma muhimu ikiwemo madawa kwa ajili ya uendeshaji shughuli za upasuaji kwa majeruhi wanaofika katika hospitali ya ya kufundishia ya Mjini Juba.