WFP yasambazia msaada wa chakula raia Sudan Kusini

24 Disemba 2013

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasambaza chakula kwa raia wa Sudan Kusini waliokimbia ghasia zinazoendelea nchini humo kwa zaidi ya wiki moja sasa. Taarifa zinasema kuwa mgao huo ulianza Jumapili kwa wananchi Elfu Thelathini waliosaka hifadhi kwenye ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS huko Juba na Bentiu.

WFP imesema mpango wake ni kusambaza chakula zaidi kwa wananchi walio kwenye maeneo mengine. Hivi sasa licha ya changamoto, WFP na wabia wake wanajitahidi kuhakikisha msaada wa chakula unafikia wale walio na mahitaji , amesema Mwakilishi mkazi wa shirika hilo n chini Sudan Kusini Chris Nikoi.  Amesema hali tete ya usalama inakwamisha jitihada zao na hivyo ameomba pande husika katika mzozo huo kulinda usalama wa raia na wafanyakazi wanaotoa misaada.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter