Mashirika ya UM yazindua mpango wa kuokoa chakula

23 Disemba 2013

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula yamezindua mpango wa pamoja wenye shabaha ya kukabiliana na tatizo la upotevu wa chakula duniani. George Njogopa na taarifa zaidi.

(Taarifa ya George)

Yote kwa pamoja, mashirika hayo lile la mpango wa chakula duniani WFP, Shirika la chakula na kilimo FAO na fuko la kimataifa la maendeleo ya kilimo IFAD yamedhamiria kutokomeza tatizo la upotevu wa chakula.

 Inakadiriwa kuwa,theluthi moja ya chakula kinachozalishwa kwa ajili ya ulaji wa binadamu kinapotea kila mwaka ikiwa ni wastani wa tani billion1.3. Kiasi hicho cha chakula kinachopotea kina uwezo wa kulisha watu bilioni 2.

Mpango huo ambao unagharimu dola za Marekani milioni 2.7 unatazamiwa kutekelezwa katika nchi tatu barani Afrika.Nchi hizo ni Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud