Zimbabwe yaandaliwa mradi wa kuendeleza kilimo

23 Disemba 2013

Shirika la misaada la Uingereza, DFID kwa kushirikiana na shirika la chakula na kilimo FAO yameanzisha mpango wa pamoja wa miaka minne kwa ajili ya kuisaidia Zimbabwe kukabiliana na tatizo la chakula kwa familia maskini. Grace na taarifa zaidi.

(Grace Taarifa)

Mpango huo ambao unakusudia kubainisha chanzo cha umaskini pamoja na tatizo la ukosefu wa chakula, pia utamulika njia bora za kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.

 Ilikufanikisha mpango huo, DFID imetenga kiasi cha dola za marekani milioni 48 kwa IFAD inayosimamia mradi wa uboreshaji wa shughuli za kilimo na maendeleo.

 Kiasi cha wakulima 300 000 wamechaguliwa ili kushiriki kwenye mradi huo ambao unatakelezwa kwa mara ya kwanza nchini Zimababwe na kukamilika kwake kunatazamia kubadili hali ya kilimo nchini humo.

Zaidi ya asilimia 70 ya wananchi waZimbabwewanategemea shughuli za kilimo kama sehemu muhimu ya kuendeshea maishayaoya kila siku. Hata hivyo wakulima hao bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa masoko na dhana duni za kilimo.