Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza Madagascar kwa uchaguzi na kuwataka kulinda amani

Ban aipongeza Madagascar kwa uchaguzi na kuwataka kulinda amani

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewaongeza wananchi wa Madagascar, tume ya uchanguzi na watu wa serikali ya Malagasy  kwa ushiriki na mchango wao katika zoezi la uchaguzi wa rais na wabunge.

Taarifa iliyotolewa leo ijumaa na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu mjini New York inasema Ban amewataka watu wa Malagasy, utawala wa mpito na wanasiasa kuendelea kutunza amani wakati wa kuendelea kuhesabu kura na kuangazwa kwa matokeo kwa awamu tofauti.  Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa unaendelea na ahadi yake ya kusaidia mafaniko ya watu wa Malagasy katika kipindi hiki cha mpito. Ban amekamilisha ujumbe wake kwa kusisitiza kuwa matakwa ya watu waMadagascarlazima yaheshimiwe.