Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa mshikamano baina ya binadamu waangaziwa nchini Kenya

Umuhimu wa mshikamano baina ya binadamu waangaziwa nchini Kenya

Tarehe 20 mwezi Disemba ni siku ya kimataifa ya mshikamano iliyoidhinishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa Disemba 22 mwaka 2005 katika azimo namba 60/ 209.  Ilibainishwa ndani ya azimio hilo kuwa mshikamano ni msingi na maadili ya kimataifa ya  kusisitiza mahusiano ya watu katika karne ya  21.

Ujumbe wa mwaka huu ni kuziba pengo ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ambapo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon amesema ni lazima kuheshimiana na kugawana majukumu ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kwa kuzingatia ahadi zilizowekwa na nchi wanachama za kutimiza malengo hayo ifikapo mwaka 2015. Hata hivyo moja ya vikwazo vikubwa vya mshikamano na utengamano ni ukabila! Mwandishi wetu Jason Nyakundi anaangazia madhara ya ukabila katika kutimiza dhana ya mshikamano ili kusonga mbele.

 (MAKALA YA JASON NYAKUNDI)