Ban awasili Ufilipino, kwenda Tacloban Jumamosi

20 Disemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko nchini Ufilipino ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemo Rais Benigno Aquino.

Habari zinasema kuwa Bwan Ban atakutana pia na wahanga wa kimbunga Haiyan au Yolanda kama kijulikanavyo nchini humo na kupatiwa taarifa kuhusu hali ya sasa ya usaidizi, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja baada ya kimbunga hicho kupiga nchi hiyo.

Jumamosi Bwana Ban ataelekea Tacloban, eneo ambalo kimbunga hicho kilisababisha madhara zaidi. Umoja wa Mataifa na wabia wake wanashirikiana na serikali ya Ufilipino kurejesha maisha ya kawaida kwa wananchi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter