Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yachukizwa na ukiukwaji wa haki Misri

Ofisi ya haki za binadamu yachukizwa na ukiukwaji wa haki Misri

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kitendo kilichofanyika huko Cairo, Misri cha kuvamia ofisi ya shirika la kiraia  linahusika na haki za binadamu na kukamatwa kwa watendaji sita kinatia hofu juu ya kuendelea kuongezeka kwa matukio hayo ya unyanyasaji dhidi ya vikundi hivyo nchini Misri.

Ofisi hiyo imesema katika tukiohilowatu waliokuwa wamevalia nguo za kiraia wakiwa na silaha ambao baadaye walitambuliwa kuwa ni askari na maafisa wa usalama walivamia kituo cha haki za binadamu na kiuchumi jumatano usiku.

Watu sita ambao walikuwa wamo kazini kwenye kituo hicho walikamatwa na yadaiwa walipigwa huku vifaa vyao vya kazi zikiwemo kompyuta tatu ndogo zikichukuliwa. Hata hivyo baadaye kompyuta mbili zilirejeshwa. Ofisi hiyo inasema wafanyakazi watano waliachiliwa huru huku mmoja aliyetambuliwa kuwa ni Mohamed Adel Fahmi akiwa bado anashikiliwa katika eneo ambalo halijulikani.