Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tushikamane, tuheshimiane tusonge mbele pamoja: Ban

Tushikamane, tuheshimiane tusonge mbele pamoja: Ban

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mshikamano, Katibu Mkuu wa UM Ban Kin Moon amesema ni lazima kuheshimiana na kugawana majukumu ili kutimiza malengo ya malengo ya milenia.

Siku hii iliyoidhinishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa December 22, 2005 ilitokana na kuzingatia kuwa mshikamano ni msingi na maadili ya kimataifa ya kusisitiza mahusiano ya watu katika karne ya 21.

Ujumbe wa mwaka huu katika siku ya mshikamano ni kuziba pengo ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Raia huyu wa Kenya anaeleza madhara ya kutoshikamana katika jamii

(Sauti Mkenya)