Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waliolazimika kukimbia makwao 2013 ilikuwa si ya kawaida: UNHCR

Idadi ya waliolazimika kukimbia makwao 2013 ilikuwa si ya kawaida: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ripoti hii leo inayosema kuwa mwaka 2013 umekuwa na idadi kubwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa na shirikahilo, la watu waliolazimika kukimbia makwao kutokana na ongezeko la wakimbizi wa ndani. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Grace)

Ripoti hiyo inasema kuwa watu milioni 5.9 walilazimishwa kukimbia makwao kwa kipindi cha kwanza cha miezi sita ikilinganishwa na watu milioni 7.6 mwaka 2012 huku nchi yenye watu waliohama wengi zaidi ikiwa niSyria. Ripoti hiyo  iliyotokana na takwimu kutoka kwa zaidi ya ofisi 120 za UNHCR  inaonyesha ongezeko kubwa kwa  idadi ya wakimbizi iliyoshuhudiwa miezi sita ya kwanza ikilingishwa na kipindi chote cha mwaka mzima uliopita. Kamishan Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres anasema kuwa itakuwa vigumu kuona watu wengi kama hao na kukosa kuuliza ni sababu  ipi inayosababisha kuhama kwa watu wengi kama hao.amesema usaidizi pekee hautoshi kumaliza tatizo bali utashi wa kisiasa ili kumaliza mizozo inayofanya watu wakimbie makwao.Afghanistaninasalia kuwa taifa ambapo wakimbizi wengi zaidi hutoka huku Pakistani ikiongoza kwa kuhifadhi wakimbizi wengi zaidi.