Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waandaa mkakati wa kipaumbele kwa haki za binadamu

Umoja wa Mataifa waandaa mkakati wa kipaumbele kwa haki za binadamu

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson, amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi kuandaa mkakati wa kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu, ambao utampa kila mmoja msukumo kufanya awezalo kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu, hususan katika mazingira ya migogoro. Bwana Eliasson ametaja mambo matatu muhimu ambayo mkakati huo unalenga kutimiza

“Kwanza ni kufanya uelezewa wa haki za binadamu uenee katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa. Pili, bila shaka, ni ulinzi wa raia- tunazungumzia wakati huu. Kuwalinda raia huwa tatizo pale tunaposhindwa kuzichukulia dalili za mwanzoni za  ukiukwaji wa haki za binadamu kwa uzingativu kama tunavyopswa kufanya. Tatu ni suala la ndani kuhusu jinsi utaratibu wetu ulivyo na maandalizi yetu kukabiliana na hali ambazo zinazobadilika kuwa janga la halaiki.”

Bwana Eliasson amesema mkakati huo umetokana na Mkataba Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mkataba wa kimataifa kuhusu haki za binadamu, pamoja na matukio kama yale ya mauaji ya kimbari Rwanda mwaka 1994, na Srebrenica mwaka 1995.

Bwana Eliasson amehoji, ikiwa ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwanzo wa jambo linaloweza kuwa janga la kibinadamu na kusababisha operesheni kuu kisiasa na katika ulinzi wa amani, ni kwa nini hatua zisichukuliwe pale ambapo tishio hilo la kuwa janga linapoanza kujitokeza?