Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tushikamane ili tufikie malengo ya milenia kwa pamoja: Rais Baraza Kuu

Tushikamane ili tufikie malengo ya milenia kwa pamoja: Rais Baraza Kuu

Mshikamano miongoni mwa watu mataifa mbali mbali duniani ni mojawapo ya fursa ya kutokomeza umaskini , amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe katika salamu zake za siku ya mshikamano duniani akirejelea lengo la kuanzishwa kwa siku hiyo.

Amesema ujumbe wa mwaka huu ni kupunguza tofauti ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015 na hata baada ya hapo, na umekuja wakati muafaka wakati baraza kuu likiwa limetenga mkutano wa 68 kuchagiza mchakato wa kufikia malengo hayo.

Bwana Ashe amesema anaamini kuwa mafanikio katika kujenga mshikamano, uwiano na haki ya kijamii yanategemea ni kwa kiasi gani tofauti baina ya nchi zinatumika kujenga uthabiti badala ya kuchochea chuki na ghasia.

Amesema haiwezi kukubalika kuendelea kuruhusu wanawake na watoto kupoteza maisha kwa magonjwa ambayo yanaepukika na kwamba mizozo, uharibifu wa mazingira lazima vikomeshwe kwani vinatishia uwepo wa wakazi wa dunia.