Wanawake wa Syria ni lazima washiriki katika kusaka amani:Brahimi

19 Disemba 2013

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu Lakdhar Brahimi amelaani hatua ya kuwafunga na kuwateka nyara wanawake wanaharakati nchiniSyria. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(Ripoti ya Jason)

Bwana Brahimi amesema kuwaSyriainapitia kipindi kigumu na wanawake wanahitaji kupewa fursa ya kusikilizwa wakati wa mpango wa amani.

Akiongea wakati wa kuanza kwa  kongamano   la wanawake waSyriamjiniGenevabwana Brahimi alizungumzia kisa ya kutoweka kwa  mwanasheria na mwanaharakati Razan Zaitouneh ambaye hajulikani halipo tangu atekwe nyara kutoka nyumbani kwake mjini Damascus majuma mawili yaliyopita. Bwana Brahimi ametoa wito kwa serikali na upinzsani kuheshimu haki za wanawake katika kupata suluhu la amani kwa mzozo ulio nchini Syria.

(Sauti ya Brahimi)

“Ninatumai kuwa wanaoshiriki katika shughuli hii wataheshimiwa na kila mmoja ikiwemo serikali na makundi ya upinzani.Hapa tutamtaja Razan Zaitouneh na wenzake watatu waliotekwa  sio muda mrefu uliopita na tunataka wao kuachilwa.Wanawake wana wajibu. Wanawake ni lazima watekeleze wajibu huo . Tunastahili kuwasaidia wanawake kwa uwezo wetu. Wanawake wana haki kama wanaume kushirikishwa, kuisaida seikali kama wanaume na kuunga mkono upinzani.”

Akiongea wakati wa kongamano hilo mkuregenzi wa wanawake wa UM Phumzile Mlambo-Ngcuka amesema wanawake na watoto wanachukua asilimia 70 ya wasyria waliolazimika kuhama makwao kutoka na mapigano.