Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM watoa ripoti kuhusu Syria na kudai “ kulifanyika mipango ya kuwadhuru raia”

Wataalamu wa UM watoa ripoti kuhusu Syria na kudai “ kulifanyika mipango ya kuwadhuru raia”

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo kuhusiana na uhalifu wa kivita uliofanyika nchini Syria imesema kuwa hakuna shaka kwamba mauwaji ya kupangilika yalifanyika.

Ripoti hiyo ambayo ni ya pili kuchapishwa ikiundwa na jopo huru la wataalamu kuhusiana na uvunjifu wa haki za binadamu nchini humo imesema kuwa vikosi vya serikali vilihusika kwa makusudi kuwashambulia raia na kuwapoteza ikiwa ni moja ya mkakati wa mapigano.

Imesema vitendo hivyo vinachukua sura ya uhalifu dhidi ya binadamu na kwamba baadhi ya raia hawajulikani waliopo na hali hiyo inatoa picha kwamba huenda wamethurika na serikali.

Tume hiyo iliendesha uchunguzi wake kuanzia March 2011 hadi Novemba mwaka huu ikiwahoji watu wa aina mbalimbali ikiwemo wale walionusurika kwenye matukio ya mashambulizi.