Baraza Kuu la OPCW lapokea ratiba ya kuteketeza silaha za kemikali za SyriaW

18 Disemba 2013

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali, OPCW, Ahmet Üzümcü amewasilisha ratiba ya mpango wa kuteketeza silaha za kemikali zaSyriakwa Baraza Kuu la shirikahilohapo jana. Mpango huo unalenga kutimiza tarehe ya mwisho ilowekwa na Barazahiloya Machi 31 2014 ya kuteketeza silaha hizo, na nyinginezo ifikapo Juni 30 mwakani.

Akilihutubia Barazahilo, Bwana Üzümcü alithibitisha kuwa mbinu muhimu za kusafirisha silaha hizo na kuzitekeza zimeandaliwa, na kwamba timu ya wataalam wanaoziteketeza wanapiga hatua muhimu hata ingawa mazingira ni magumu.

Amesifu nchi wanachama wa OPCW kwa kutoa vifaa vya usafirishaji na vya kuziteketeza silaha hizo, pamoja na usaidizi wa aina nyingine, ukiwemo wa kifedha.

Hata hivyo, Bwana Üzümcü ameonya kuwa ratiba hiyo imekumbana na matatizo ya kiusalama, utaratibu wa kutoa idhini za kimataifa za usafirishaji na hata hali mbaya ya hewa, na kuongeza kuwa huenda kukawa na kuchelewa kidogo.