Mjumbe wa UM asema kuwa Korea Kaskazini imetekeleza mauaji ya watu mashuhuri

18 Disemba 2013

Mtaalamu wa haki za bindamu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa kunyongwa kwa  afisa wa ngazi ya juu nchini Korea Kaskazini ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.

Marzuki Darusman amesema kuwa kukamatwa, kuhukumiwa na kunyongwa kwa Jang Song Thaek mjombake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ni kitendo ambacho kilifanyika kwa kipindi cha kati ya siku tano.

Kunyongwa huku kuliripotiwa na vyombo vya habari vya taifa ambapo iliripotiwa kuwa Jang Song Thaek alipanga kuipindua serikali.  Darusman amesema kuwa amepokea habari za kunyongwa kwa watu hadharani nchini Korea Kaskazini kutokana na makosa yanayohusiana na kuuza kanda haramu za video, Kutizama video za ngono na matumizi ya madawa ya kulevya.