Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waelezea hofu kufuatia ghasia Somalia

Umoja wa Mataifa waelezea hofu kufuatia ghasia Somalia

 

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay, ameelezea hofu yake kuhusu machafuko ya hivi karibuni nchini humo.

(Taarifa ya Grace)

Bwana Kay amesema machafuko yaliibuka katika maeneo kadhaa ya nchi huenda yakatishia barabara ya hatua za kuweka amani na utulivu, pamoja na haki za maelfu ya raia walioathirika.

Ghasia zimeripotiwa karibu na Johwat katikati mwa Shabelle, maeneo ya Beledweyne Hiraan na karibu K50 Shebelle Kusini.

Ripoti zinasema kuwa wanamgambo wa kikaya wanawafurusha wakulima na wanavijiji kutoka kwa mashamba wanapopanda mimea. Machafuko hayo yameelezwa kusababisha vifo, majeraha, kuwalazimu watu kuhama makwao na uharibifu wa mali na mimea mashambani. Wanaoathiriwa zaidi hutoka kwenye jamii au kaya zenye watu wachache zaidi.