Rider ,Pillay watambua mchango wa wahamiaji duniani

18 Disemba 2013

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani ILO  Guy Rider pamoja na Kamishna wa haki za binadamu Navi Pillay  wametoa heshima zao kwa wahamiaji zaidi ya milioni 232 duniani kote ambao kwa nyakati tofauti waliondoka toka maeneo yao ya asili na kwenda sehemu za mbali kwa ajili ya kusaka fursa zaidi.

Wakuu hao wamesema kuwa wahamiaji hao wanaendelea kutoa mchango mkubwa kwa uchumi na maendeleo ya kijamii kwa ujumla katika nchi wanazofikia na kule walikotoka.

Lakini pamoja na mchango huo mkubwa lakini bado haitambuliwi na badala yake wanakumbana na vitendo vya ubaguzi na kutengwa.

Wametoa wito wakitaka kuondolewa kwa kadhia zinazowaandama wahamiaji hao na zaidi ya yote wametaka kuwepo kwa maingiliano ya kijamii na mshikamano wa pamoja.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud