Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Magharibi ina uwezo wa kuimarisha sekta ya kilimo:FAO

Afrika Magharibi ina uwezo wa kuimarisha sekta ya kilimo:FAO

Utafiti mpya uliotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO  na lile la IFAD umeonyesha kuwa kuimarisha kwa shughuliza za uzalishaji na ushindani pamoja na kuwajengea uwezo wakulima wadogo wadogo ni mambo muhimu yanayoweza kutoa msukumo mkubwa wa kuwa na kilimo hai katika nchi za Afrika Magharibi. George Njogopa na taarifa kamili.

 (Taarifa ya George)

Utafiti huo umeonyesha nyanja mbalimbali za mafanikiwa tangu eneo hilo lilipoweka msukumo mpya kwa kuwekeza kwenye maendeleo ya kilimo ikiwa ni jaribio la kukabiliana na kitisho cha njaa kilichoikumba dunia katika msimu wa mwaka 2007-2008.

Hata hivyo katika utafiti wake huo mashirika hayo ya kimataifa yamesema kuwa nchi hizo zinaweza kunufaika zaidikama zitaweka mkazo kwenye maeneo ya sera.

Mashirika hayo yanazitaka nchi hizo kuanzisha agenda ya kuzipiga jeki sera zinazohimiza maendeleo ya kilimo ikiwemo pia kuzingatia mfumo wa ushirikiano baina ya sekta binafsi na zile za umma.

Kulingana na Mwanauchumi mwandamizi wa FAO Aziz Elbehri ambaye ndiye aliyehariri ripoti ya utafiti huo anasema kuwa kuongeza upendeleo kwenye maeneo ya sera na masoko kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ushindani kwa wakulima wadogo jambo ambalo litaongeza nafasiyaokwenye soko

 (Sauti ya Elbehri)