Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa usaidizi kwa Haiti kwa 2014

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa usaidizi kwa Haiti kwa 2014

Huko Geneva, Umoja wa Mataifa umezindua mpango wa mwaka ujao wa usaidizi kwa Haitiwa dola Milioni 169 kwa ajili ya wakazi Laki Nane wa jamii 35 kati ya 140 za nchi hiyo

Mwakilishi mkazi wa usaidizi wa kibinadamu nchiniHaiti, Peter de Clercq amewaambia waandishi wa habari kuwa nusu ya fedha hizo ni kwa ajili ya mahitaji ya kimsingi ya wakazi 145,000 wanaotarajiwa kuwepo bado kwenye kambi mwakani tangu tetemeko kubwa la ardhi nchini humo la mwaka 2010, mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kimbungaSandy.

Bwana Clercq amesema ni vyema kutambua mafanikio makubwa yamepatikana ya usaidizi baada ya majanga hayo kutokana na jitihada za pamoja za serikali, mashirika ya kiraia na jamii ya kimataifa lakini lazima kuwa macho..

(Sauti ya Clercq)

 

“Takribani asilimia 30 ya wananchi Milioni 10 wa Haiti bado wanakabiliwa na uhaba wa mahitaji ya msingi. Watu 145, 000 bado ni wakimbizi wa ndani na wanaishi kwenye kamb, wengi wao ni wanawake na watoto wakiwa hawana pahala pa kwenda na hawana mwelekeo wowote! Wanaishi kwenye mahema ambapo choo kimoja kinatumiwa na watu 50. Hawana kabisa au wana huduma duni ya afya, maji na elimu. Suluhisho la tatizo hilo liko bayana na linaweza kupatikana iwapo fedha hizo za usaidizi kwa mwaka 2014 zitapatikana.”

 Bwana De Clercq amesema ilhali majawabu ya kudumu yanaendelea kusakwa kwa maslahi ya wananchi waHaiti, ulinzi kwenye kambi unasalia kuwa kipaumbele kwani wakimbizi hao wako hatarini kufukuzwa kutoka kambini.