Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali nchini Afghanistan

17 Disemba 2013

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali nchini Afghanistan katika muktadha wa amani na usalama wa kimataifa. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Mkutano huo wa Baraza la Usalama umehutubiwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA, Jan Kubis ambaye ameelezea umuhimu wa kuendelea kufanya kazi pamoja, ili kuhakikisha kuna taifa huruna endelevu la Afghanistan, ambalo halitakuwa tena hifadhi ya ugaidi wa kimataifa na uhalifu wa kupangwa, hususan ikiwemo ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Bwana Kubis pia amezungumza kuhusu umuhimu wa kufanya uchaguzi wa kuaminika haraka, na ambao unazingatia misingi ya kikatiba.

“Maandalizi ya kitaaluma na kasi ya kisiasa kwa uchaguzi wa tarehe ilokubaliwa ya Aprili 5, bado ni mazuri  hata zaidi ya uchaguzi wa zamani. Changamoto za kisiasa ni dhahiri na zinatakiwa zikabiliwe kwa njia bora ili kuendeleza ujumuishaji kamilifu na kuepusha sababu yoyote ya kuwanyima watu kupiga kura, au kuchelewa. Haya yanajumuisha uwazi kuhusu sehemu za kupiga kura na maamuzi muhimu yatakayofanywa siku zijazo.”

Bwana Kubis amesema anataraji uchaguzi huo na mazingira yaliyopo ya kisiasa, vitaongeza umoja wa kitaifa, na sio kuongeza chuki za kidini na migogoro